Kitauli afunguka kuhusu Maisha yake ya Mziki
Msaani Beatrice kitauli ni mojawapo ya wasaani ibuka katika tasnia ya Mziki ya inijili kule Tanzania , amepata fursa ya kufanya kazi na msaani tajika Rose Muhando .Beatrice anatupa taswira ya maisha yake kwenye idhaa ya habari Shemeza cloud news.
Kwa kifupi Beatrice kitauli ni nani?Ni Mwimbaji wa Nyimbo za injili ambaye ni mwenyeji wa Tanzania. Aliyeanza kuimba kwenye Kwaya tangu mwaja 2006 na baadae kuimba kama Mwimbaji binafsi mnsmo mwaka 2012
Ni nini kilichokuchochea kuanza uimbaji wa nyimbo za injili ? Kuimba ni kitu napenda toka moyoni na ni kusudi LA Mungu aliloniumba nije nitimize. Yaani kuhubiri injili kwa njia ya uimbaji
Changamoto zipi unakumbana nazo? Changamoto ni nyingi ila kubwa ni kipato kuwa kidogo ambapo nashindwa kutekeleza baadhi ya mambo mengi yanaohusu uimbaji
Kama mwanamziki nini unazingatia katika uandishi wa nyimbo zako?Huwa nazingatia sana kuongozwa na roho mtakatifu, ambapo ananiongoza katika kuandika mashairi yenye ujumbe, pia nazingatia aina ya watu wanaokwenda kupokea ujumbe huo na Mara nyingi nazingatia kutumia maneno ya kwenye biblia katika nyimbo ambayo ndio injili hasa. Kikubwa nalenga kuandika Nyimbo zitakazobadilisha maisha ya watu kutoka mabaya kwenda mazuri yanayompendeza Muumba
Umefanya collabo na Rose muhando , mulipatanaje na mbona mukafanya ushirikiano?Rose Muhando nilikutana naye studio nikamwomba na nilimwambia nilitamani sana kufanya naye uimbaji akanikubalia… Nilichopenda kutoka kwake ni ile kujituma kwake kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii, bila dharau wala majivuno na kwa kujishusha na kuheshimu watu wote
Tutajie baadhi ya nyimbo zako ?Nimetoa albamu tatu hadi sasa ya kwanza inaitwa umeniinua, ya pili inaitwa usiguse utukufu wa Mungu, na hii ya Tatu inaitwa Maua. Katika album hii ya tatu kuna Nyimbo tatu tu ambazo zipo zimesambazwa ambazo ni Wimbo wa Maua, Wimbo wa Kesho niliyoimba na rose Muhando pamoja na Wimbo unaitwa Wajue ambapo nimeimba pia na Rose Muhando
Mwaka huu umeachilia bonge LA kazi tueleze zaidi kulihusu? Ohoo huu ni muendelezo wa Nyimbo ambazo zipo kwenye Albam ya Maua. Ambayo bado kumalizika ni Wimbo wa 3 kwenye Albam hii
Ungepewa fursa ungebadili nini ? Ningepewa fursa ya kubadilisha kitu nisingebadilisha kitu. Mimi naona kwa upande wangu mambo yako vile Mungu alipanga…. Maana kila kitu naamini ni mipango ya Mungu
Unamtazamo UPI kuhusiana na Mziki wa afrika mashariki? Kwa mtazamo wangu, mziki wa Africa mashariki unatakiwa kukua maana naona kama wadau wa muziki wamepoa. Tunatakiwa tuwe na watu wengi tutakaosaidiana nao hasa kufanya kwa mfano Nyimbo za laivu. Lakini ukiangalia maeneo mengi hakuna sapoti ya vyombo vya muziki vizuri vinavyospoti waimbaji kuimba laivu
Ni msaani yupi unahamu ya kufanya naye kazi?Ni wengi sana na sio mmoja. Natamani kuimba na mercy masika Kenya, Christina Shusho na wengine. Hata woote kama ningekuwa na uwezo.
Ni nini kinafanya Mziki wako uwe tofauti na ya wasaani wengine ? Kinachofanya muziki naofanya kuwa tofauti ni kwamba napenda kutumia sauti yangu asili aliyonipa Mungu na napenda kufanya kama Mimi na napenda zaidi kutumia mapigo ya ngoma za asili mfano Wimbo wa Maua
Mafans wako watarajie nini?Watarajie kupata Nyimbo nyingine 3 ambapo zinakamilishwa zinazokmilisha Albam ya Maua itakayokuwa iko kwenye mfumo wa Audio na video. Kikubwa nawaomba waIngatie zaidi ujumbe uliomo ndani ya Nyimbo hizo ili ujumbe uwafae maishani.
Wosia yako kwa wasaani ibuka?
Napenda kuwapa ushauri kwamba ikiwa mmoja ameamua kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji, basis ajitoe kimwili na kiroho na pia awekeze kwa udhubutu ili injili isonge mbele maana kwenye injili kunahitaji uwekezaji pia.
Wajiona ukiwa wapi miaka 5 zijazo ?Najiona nikiwa wa kimataifa zaidi na nikiwa nimeyatimiza baadhi ya malengo yangu niliyopanga katika kumtumikia Mungu.